MARKAZ IMAMUL BUKHARIY (رحمه الله تعالى)
SOKOMATOLA - BARABARA YA 5-JIJINI MBEYA
Hii ni Markaz Kongwe ya Masalafiy wa Jiji la Mbeya iliyoanzishwa Maalumu kuwasaidia vijana wanaotoka nyanda za juu kusini hasa wale wanaoisilimu kusoma dini kwa walimu wa kisalafi na kurudi mikoani mwao wakiwa walinganizi wa dini ya Allah سبحانه وتعالى.
HISTORIA FUPI YA MARKAZUL IMAMIL BUKHARIY
Markaz hii iliasisiwa na kuanzishwa na viongozi wa Masjidul Imamil Bukhariy wanaitwa "watu wa Shura ya Msikiti" kati ya mwaka 2007 mapaka 2009. Toka miaka hiyo wanafunzi wamekuwa wakichukuliwa na kulelewa na Msikiti bila malipo yeyote mpaka leo hii,ولله الحمد والمنة .
Markaz imekuwa ikuchukuwa wanafunzi kati ya kumi mpaka kumi na tatu kwa muhula wa masomo kila mwaka na idadi hii inatokana na ufinyu wa eneo la Msikiti sambamba na mabweni ya wanafunzi.
WALIMU WALIOWAHI KUPITA KUSOMESHA MARKAZUL IMAMIL BUKHARIY
1 - Abuu Laylah Richard Zunda ambaye ndiye Mudiri wa Markaz toka 2011 mpaka hivi leo
2 - Abuu Haafidh Maulid (Mwanafunzi wa Markazul Bukhariy aliyekuja kuwa mwalimu Baadae)
3 - Abuu Muadh (Mwalimu toka Songea aliyekuja Mbeya kwa ajili ya kusomesha dini toka mwaka 2021 ndio msimamizi wa markaz mpaka hivi leo).
4 - Abuu samak Ibrahim Ally (Msimamizi wa Taaluma wa Markaz tokea mwaka 2014 mpaka hivi leo).
5 - Ustaadh Khamis Imam Mkuu wa Masjid Imamul Bukhariy (Aliwahi kuwa mwalimu wa wanafunzi wa Markaz kwa muda kisha akashika majukumu mengine ya Taaluma kwa watoto wadogo Masjid Imamul Bukhariy).
WALIMU WALIOWAHI KUPITA MARKAZ KTK MUDA TOFAUTI WAKATOA FAIDA NA KUSOMESHA VITABU AU BAADHI YA MILANGO KATIKA VITABU KWA WANAFUNZI WA MARKAZ
1- Abuu Umeyr Adam Khamis kutoka Masjid Faaroq Mkele Zanzibar.
2- Abuu Raslaan Mussa Kilongozi kutoka Markaz Imam Maalik Dodoma.
3-Abuu Anas Ismail Kizza kutoka Markaz Ibn Taymiyyah Pongwe.
4-Abuu Fat'hiyah Kizza Kutoka Markaz Ibn Uthaymeen Dodoma
5-Abuu Abdillah Kutoka Nzega
6-Abuu Dhannun kutoka Markaz Imamu Shaafi songea
7-Abuu Musa Kiza kutoka Markaz Ahlusunna Tabora
8 - Abuu Khaulah Assed Kutoka Kizimkazi, Zanzibar.
9-Abuu Zakaria Al hanbally kutoka Zanzibar
10- Ustadh Shu'ayb Imamu mkuu Msikiti wa Must-Mbeya.
Alhamdulilah kwa Neema yake Allah kwetu.
Namba zilizoandikwa nyuma ya majina ya Walimu na Maduati waliopita Markaz haziakisi ubora baina yao bali ni kujulisha idadi na si vinginevyo.