DARSA ZA MARKAZ ZOTE MBEYA

Assalamu Alaykum! Endapo kutakuwepo na darsa ya live tutajuilishana

MARKAZ IMAM MUSLIM

Card image

MARKAZ IMAM BUKHARI

Card image

MARKAZ IMAM DAUD

Card image

content2

MARKAZUL IMAMIL BUKHARIY - SOKO MATOLA MBEYA MJINI

MARKAZ IMAMUL BUKHARIY (رحمه الله تعالى)

SOKOMATOLA - BARABARA YA 5-JIJINI MBEYA

Hii ni Markaz Kongwe ya Masalafiy wa Jiji la Mbeya iliyoanzishwa Maalumu kuwasaidia vijana wanaotoka nyanda za juu kusini hasa wale wanaoisilimu kusoma dini kwa walimu wa kisalafi na kurudi mikoani mwao wakiwa walinganizi wa dini ya Allah سبحانه وتعالى.

 HISTORIA FUPI YA MARKAZUL IMAMIL BUKHARIY

 Markaz hii iliasisiwa na kuanzishwa na viongozi wa Masjidul Imamil Bukhariy wanaitwa "watu wa Shura ya Msikiti" kati ya mwaka 2007 mapaka 2009. Toka miaka hiyo wanafunzi wamekuwa wakichukuliwa na kulelewa na Msikiti bila malipo yeyote mpaka leo hii,ولله الحمد والمنة .

Markaz imekuwa ikuchukuwa wanafunzi kati ya kumi mpaka kumi na tatu kwa muhula wa masomo kila mwaka na idadi hii inatokana na ufinyu wa eneo la Msikiti sambamba na mabweni ya wanafunzi.

 WALIMU WALIOWAHI KUPITA KUSOMESHA MARKAZUL IMAMIL BUKHARIY

1 - Abuu Laylah Richard Zunda ambaye ndiye Mudiri wa Markaz toka 2011 mpaka hivi leo

 2 - Abuu Haafidh Maulid (Mwanafunzi wa Markazul Bukhariy aliyekuja kuwa mwalimu Baadae)

3 - Abuu Muadh (Mwalimu toka Songea aliyekuja Mbeya kwa ajili ya kusomesha dini toka mwaka 2021 ndio msimamizi wa markaz mpaka hivi leo).

4 - Abuu samak Ibrahim Ally (Msimamizi wa Taaluma wa Markaz tokea mwaka 2014 mpaka hivi leo).

 5 - Ustaadh Khamis Imam Mkuu wa Masjid Imamul Bukhariy (Aliwahi kuwa mwalimu wa wanafunzi wa Markaz kwa muda kisha akashika majukumu mengine ya Taaluma kwa watoto wadogo Masjid Imamul Bukhariy).

WALIMU WALIOWAHI KUPITA MARKAZ KTK MUDA TOFAUTI WAKATOA FAIDA NA KUSOMESHA VITABU AU BAADHI YA MILANGO KATIKA VITABU KWA WANAFUNZI WA MARKAZ

1- Abuu Umeyr Adam Khamis kutoka Masjid Faaroq Mkele Zanzibar.

 2- Abuu Raslaan Mussa Kilongozi kutoka Markaz Imam Maalik Dodoma.

3-Abuu Anas Ismail Kizza kutoka Markaz Ibn Taymiyyah Pongwe.

 4-Abuu Fat'hiyah Kizza Kutoka Markaz Ibn Uthaymeen Dodoma

5-Abuu Abdillah Kutoka Nzega

6-Abuu Dhannun kutoka Markaz Imamu Shaafi songea

7-Abuu Musa Kiza kutoka Markaz Ahlusunna Tabora

8 - Abuu Khaulah Assed Kutoka Kizimkazi, Zanzibar.

9-Abuu Zakaria Al hanbally kutoka Zanzibar

10- Ustadh Shu'ayb Imamu mkuu Msikiti wa Must-Mbeya.

Alhamdulilah kwa Neema yake Allah kwetu.

Namba zilizoandikwa nyuma ya majina ya Walimu na Maduati waliopita Markaz haziakisi ubora baina yao bali ni kujulisha idadi na si vinginevyo.

HALAQAAT

MARKAZUL IMAMI MUSLIM - TAHFEEDH.

MARKAZUL IMAMI MUSLIM (رحمه الله) - TAHFEEDHUL QUR'AN.

ISYESYE-MAJENGO MAPYA-JIJINI MBEYA

Chuo Cha Kwanza cha Masalafiy Nyanda za juu kusini ikijumuisha mikoa ya Mbeya,Iringa,Rukwa,Songwe na Ruvuma kujikita katika kuhifadhisha Qur'an.

Markazil Imam Muslim Isyesye - Mbeya Mjini ni Chuo Maalumu cha Masalafi wa Jiji la Mbeya kilichojikita katika kuhifadhisha Qur'an.

HISTORIA YA CHUO HIKI: Asili ya Markaz hii inarudi mpaka mwaka 1439/2018 pale Masalafiy wa jiji la mbeya walipokaa kikao na kuazimia kwa pamoja kuanzishwa kituo Maalumu cha Masalafiy wa jiji la Mbeya, na katika Maazimio ya kikao hicho ni kuanzishwe group la WhatsApp ambalo litasimamia michango ya waislamu ili tuweze kununua kiwanja na baadae ujenzi uendelee.Hivyo basi Ilipofika tarehe 30 November 2018 likaanzishwa rasmi Group lililotwa "UJENZI MARKAZ MBEYA" Kwa Neema yake Allah Group hili lilifanikisha ununuzi wa kiwanja cha Markaz kilichopo Isyesye Majengo mapya na Ujenzi wa Msikiti ambao mpaka ulianza kufanya kazi kwa mara ya kwanza kwa kuchukua wanafunzi wa kulala bweni 5 Dhul Qaadah 1443/4 June 2022.

Markaz hii ilianza rasmi kuchukua wanafunzi wa bweni mwaka 1443-1444/2022-2023 na walipatikana wanafunzi 10 toka sehemu mbalimbali za Tanzania na watano katika hao walitoka Markaz Imamul Bukhariy -Soko Matola Mbeya Mjini, na Muhula wa masomo uliofata mwaka 1444-1445 sawa na 2023-2024 Markaz ilisajili wanafunzi 35 toka sehemu mbali mbali za Tanzania.

 Licha ya Tahfeedh Markaz inahifadhisha bali pia imekuwa ikisimamia Darasa za Quran na Elimu ya dini kwa Kina Baba na kina Mama na watoto wadogo.

 WALIMU WALIOWAHI KUSOMESHA MARKAZ IMAM MUSLIM VITABU AU MILANGO MBALIMBALI KATIKA DINI.

 1-Abuu Umeyr Adam Khamis Az-Zinjibaar.

2- Abuu Fauzan Muhammad Sulayman Al bimani

3-Abuul Mundhir Saddaam (Miongoni mwa wanafunzi wa Markaz)

4-AbuuSamak Ibrahim Aliy Mkate (Mudir wa Markaz)

 WALIMU WALIOSIMAMIA MADRASA YA WATOTO

 1- AbulAbbas Ashraf.

2- Omar Michael Sesaguli (Alisilimu Mwaka 2017 Shinyanga Tanzania).

VIONGOZI WA MARKAZ

Mudir wa Markaz: Abuu Samak Ibrahim Mkate 0717600999

Mwalimu wa Tahfeedh: Abu Salmaan Saalim Habib Az-Zinjibariy wakisaidiana na Abuu Fauzan Muhamad Sulayman Al Bimani.

QUR-AN TAHFEEDH

MARKAZIL IMAM ABIY DAUWD ASSIJISTAANIY - MBALIZI

MARKAZUL IMAM ABIY DAWUUD ASSIJISTAANIY - MBALIZI

Markaz hii ni zao la durus na Halaqaat za Markazil Imamul Bulkhariy Soko matola,Jijini Mbeya, pale walipopatikana wanafunzi wakiongozwa na Abuu Muhamad Yazid wakaanzisha harakati za kupatikana kwa msikiti Mbalizi na jambo hilo limefanikiwa kwa kupata Uwanja ambao mwaka huu (1445/2024) Inshaallah mwezi wa sita ujenzi unatarajiwa kuanza.

 DURUUS KATIKA NYUMBA ZA WATU MBALIMBALI MBALIZI ZINAENDELEA NA HAWA NI WALIMU WALIOWAHI KUSOMESHA.

 1- Abuu haafidh Maulid

2- Abdulkarim wa Shinyanga

3- Muhamad wa Mwanza

4- Abuu Muhamad Yazid wote hawa ni wanafunzi waliowahi kupita Markazil Imam Bukhariy,Soko Matola Mbeya Mjini.

 

HALAQAAT

MASOMO YANAENDELEA

Assalamu alaykum warahmatullah,

MUNAKUMBUSHWA MARKAZ IMEFUNGÙLIWA,


27 shawwaal 1445


MASOMO YANAENDELEA

Assalamu alaykum warahmatullah,

MUNAKUMBUSHWA MARKAZ IMEFUNGÙLIWA,


27 shawwaal 1445


Suratul Al-Furqaan


Maelezo:

maelezo

UCHUMBA NDANI YA UISLAMU

gngnghv

hghghghg

UCHUMBA NDANI YA UISLAMU

fggffgfgfg

hgfghjhgf

UCHUMBA NDANI YA UISLAMU

hgjgjgh

hgjgh

JJHHJ

fggffgfgfg

ddddddddddd

UCHUMBA

MAS’ALA YA KWANZA : MCHUMBA KUMUONA ANAEMCHUMBIA 

Amesema sheikh muhamad bin saalih al uthaymeen حفظه الله katika kadhia hii ya kwamba Inafaa kwa mchumba kumuona anaemchumbia Kwa haja maalum ya kumfaham akishamuona na akaridhika kumuoa-haina haja ya kurudia rudia kumuangalia kwa sababu bado hajamuoa

TANBIHI:
-Na  hii tofauti kabisa na mazoea tulionayo mtu akichumbia ndo inakuwa sasa kana kwamba kaoa,kila muda anataka muona,wengine mapicha kutumiana,mara kugusana gusana ni mambo ambayo hayafai watu wafanya kwa kigezo uchumba/hayapo hayo.
-Wengine utaona wanaenda beach na hao wachumba,mara mwanamke anamtembelea mwanaume kwao au alikopanga,hakika tumche ALLAH ikhwa na kufata mwenendo wa MTUME صلى الله عليه وسلم.
Soma zaidi